Habari na Paul Manjale
Kiungo mpya wa klabu ya Chelsea Muhispania Cesc Fabregas (27) ameweka
rekodi mpya katika ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Backleys Premier League
baada ya kutoa pasi sita za magoli katika michezo sita mfululizo ya ligi hiyo.
Fabregas ameweka rekodi hiyo kufuatia pasi mbili alizotoa kwa
mshambuliaji Diego Costa dhidi ya
Swansea,moja dhidi ya Everton na moja nyingine dhidi ya Leicester City na mbili
dhidi ya Burney wiki kadhaa zilizopita huku mwaka 2011 akiiaga ligi hiyo kwa
pasi nyingine tatu dhidi ya Bolton na Tottenham akiwa na jezi ya Arsenal kabla
ya kutimkia Barcelona.
Wakati Fabregas akiweka rekodi hiyo ya aina yake,watambue nyota wengine watano walioweka rekodi ya kufumania
nyavu katika michezo mitano mfululizo ya Backleys
Darren Anderton – Spurs,1992/93
Gianfranco Zola – Chelsea,2002/03
Ryan Giggs – Man United,2002/03
Thierry Henry – Arsenal,2004/05
Antonio Valencia – Man United,2011/12
0 comments:
Post a Comment