Kocha mwenye tambo na
maneno mengi Mreno Jose Mourinho ameibuka na kudai kuwa kocha wa klabu ya
Bayern Munich Muhispania Pep Guardiola ananyonyoka nywele na kubaki kipara
kwasababu haenjoy (hafurahii) mchezo wa soka kama yeye.
Mourinho ameyatoa maneno
hayo baada ya wawili hao kuibua ubishani
wakati wa mkutano wa makocha uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya UEFA kujadili
urefu wa nyasi viwanjani.Habari zinasema mzozo huo ulianza baada ya Guardiola
kusisitiza kuwa urefu wa nyasi usizidi sentimeta 1.5 ili kuufanya mchezo uwe na
kasi na mvuto.
Kufuatia maoni hayo
Mourinho alipinga na kusema “Kila
mtu ana aina yake ya uchezaji,ambayo inapaswa kuheshimiwa.Soka inaweza
ikawa na mvuto kwa njia nyingi.
Guardiola akajibu “Uzuri wa soka unategemea timu inafundishwa na kocha
yupi.Inaonekana Mourinho anapendelea zaidi matokeo kuliko mvuto/uzuri.
Baada ya maneno hayo
Mourinho alijibu mapigo kwa kusema “Unapofurahia/enjoy kile unachokifanya huwezi kunyonyoka nywele na
Guardiola ana uwalaza/upara ni kwasababu hafurahii soka.
0 comments:
Post a Comment