Habari na Paul Manjale
Timu ya taifa ya
England imeanza vizuri kampeni yake ya kuisaka tiketi ya kushiriki michuano
ijayo ya Ulaya (Euro 2016) baada ya kuibamiza timu ya taifa ya Uswisi kwa jumla
ya mabao 2-0.
Welbeck akishangilia goli la pili dhidi ya Uswisi |
England ilijipatia
magoli yake kipindi cha pili cha mchezo huo wa kundi E uliopigwa katika dimba
la St Jacob Park mjini Basel kupitia kwa mshambuliaji wake Danny Welbeck dakika
za 59 na 90 akitumia vyema pasi za winga Raheem Sterling.
Welbeck akifunga goli la kwanza |
Baada ya mchezo huo
kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson aliwasifu wachezaji wake na
kusema wameutendea haki mfumo wa 4-4-2 diamond huku pia akionyesha ishara ya
dole gumba kwa viungo wake Jack Wilshere,Raheem Sterling na Fabian Delph na
mlinzi John Stone kwa kuonyesha soka safi na kuifanya timu icheze kwa uelewano
mkubwa.
Kocha Hodgson akishangilia moja kati ya magoli dhidi ya Uswisi |
Huu ni mchezo wa kwanza
kwa timu ya taifa ya Uswisi inayonolewa na kocha Vladimir Petkovic kupoteza
ikiwa nyumbani baada ya kufanya hivyo miaka minne iliyopita kwa kufungwa na
England Oktoba mwaka 2010 kwa jumla ya magoli
3-1.
0 comments:
Post a Comment