728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 12, 2014

    TAYARI KUNA MAKUNDI MAWILI NDANI YA MSIMBAZI

    NINAVYOAMINI MIMI

    Na: Bakari Ally
    Simu: 0682004504


    Wakati nikiwa nyumbani wiki kama tatu nyuma nikiwa naumwa nilimuagiza rafiki yangu mmoja akienda mjini akirudi anichukulie gazeti la mwanasporti na nilikuwa na sababu kuu mbili ndio maana nimuagize gazeti la mwanasporti kwanza kabisa nilitaka habari ya patrick phiri juu ya ujio wake mpya simba sports club pia nilitaka kuangalia tetesi za usajili majuu zinaendeleaje?


    Rafiki yangu baada ya kuzunguka mizunguko yake ya siku mzima ndipo jioni akawa amerudi na kuniletea gazeti la mwanasporti tena lilikuwa la siku hiyo hiyo ni Ijumaa tarehe 15/08/2014 kwa kuliona gazeti hata nafuu nikapata nikaamua kuchukua lile gazeti lakini nje nikiona kichwa cha habari kikubwa kinasema "YANGA LAZIMA WAKAE" Huku kukiwa na picha ya patrick phiri nikasema hii ndio habari ninayohiitaji.



    Ile habari iliandikwa ukurasa wa pili katika kusoma ile habari mwishoni nikaona maneno ya Rais wa Simba SC Evans Aveva akisema "Tumempa kocha mkataba wa mwaka mmoja,lengo kubwa kwetu ni kutengeneza timu ya ushindani,tungemwambia atwae ubingwa kwa msimu ujao lakini tumefanya tathimini na kuona kikosi cha timu yetu kinahitaji kutengenezwa ili kiwe cha ushindani.Tunaamini kazi hiyo yeye anaiweza ndio maana tumeamua kuwa nae".
    Nikawa nimejiuliza msimu uliopita King Kibadeni alipewa atengeneze timu lakini baadae akatimuliwa wakasema wanataka kombe je watamvumilia phiri? Pia nikawa na swali kujenga timu unapitia kwenye kipindi cha tabu kweli watavumilia?


    Mechi takribani nne za kirafiki simba wamecheza huku wakionyesha mpira mkubwa kabisa na kushinda mechi zote wameshinda 2-1 dhidi ya Shangani,2-0 dhidi ya Mafunzo na 5-0 dhidi ya KMKM na pia juzi tumeona wakishinda 3-0 dhidi ya Goh mahia.

    Kwa matokeo hayo tangu aje patrick phiri baadhi ya mashabiki,wadau na viongozi wa simba wameshaachana na mawazo ya kutengeneza timu akili yao sasa ni ubingwa wa V.P.L kwahiyo kwa sasa simba kuna makundi mawili wale wakina Evans Aveva ambao wanataka watengeneza timu na kuna lile kundi hao hawajui chochote ile dhana ya kujenga timu imekufa wanataka wachukue ubingwa.


    Kuwepo kwa makundi hayo mawili tayari kuna hatarisha hata nafasi ya patrick phiri kuwepo klabuni hapo kama ataboronga kama ilivyokuwa kwa Van Gaal hapa nitaona mabango kuwa Phiri hatakiwi kwa kuwa kuna wadau washabiki na viongozi wameshakuwa na dhana ya kuwa timu yao ni mzuri imekamilika kila idara unaweza sema simba imekamilika mechi nne goli 12 na wameruhusu goli 1 lakini muda kuwa timu yenye ushindani bado.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAYARI KUNA MAKUNDI MAWILI NDANI YA MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top