728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 10, 2014

    HIVI ANKO HAO JAMAA MBAKUSHOBOROLA BATAI?



    MAKALA YA LEO:

    Allen kaijage
    0655106767
    kaijagejr@gmail.com

     


                            
    Hakuna kitu kigumu kama kufanya uchaguzi wa vitu vichache katika vingi.Ili kufanya uchaguzi sahihi wanauchumi hutumia kanuni inayoitwa scale of preference(kuchagua kitu au vitu katika vitu vingi kutokana na umuhimu wa mahitaji yako).Kwenye scale of preference utafanya uchaguzi kuanzia kwenye kitu muhimu kabisa alafu vingine hufuata.Kama unataka kuchagua bidhaa lazima uchague kulingana na mahitaji yako muhimu alafu bidhaa kwa ajili ya mahitaji ya ziada zitafuata.

    Hata kwenye uchaguzi wa marafiki na wasaidizi lazima tutumie kanuni hii ya wachumi.Ukitaka kuchagua marafiki lazima upime umuhimu wa hao watu unaotaka kuwafanya rafiki zako.Sasa hapo kila mtu huwa na uhitaji wake.Utachagua rafiki kutokana na sifa za uhitaji wako.Mwenye sifa za kutosha ndio utampa kipaumbele.Vivo hivyo kwenye kuchagua wasaidizi wa kazi lazima uwachague watu kutokana na kazihusika.Huwezi kumchagua daktari kwenye kazi ya ujenzi kisa huyo daktari ni mchapa kazi hospitali,Au umchague mwalimu kwenye kazi ya uhasibu kwasababu tu mwalimu huyo unamfahamu.Hapo utajikaanga kama nguruwe.Kwani mwalimu hawezi kukupa ushauri mzuri wa maswala ya fedhakama muhasibu aliyesomea uhasibu pia daktari hawezi kukupa ushauri mzuri wa maswala ya ujenzi kama atakavyokupa muhandisi.
     
    Hapa ndipo Watanzania wengi tunafeli,Mara nyingi hatufanyi uchaguzi sahihi.Watu wengi tumeweka wasaidizi wa kazi wasio na ujuzi Mkubwa kwenye kazi husika.Watu wengi wameweka undugu na urafiki mbele katika kazi ndio maana hatuendelei.Mtu anafanya kazi
    kwasababu bosi wake ni Mtoto wa baba ake mdogo.Sikatai kumuweka mtu kwasababu ni ndugu yako au rafiki yako,Bali nakataa uwepo Wa ndugu au rafiki asiye na taaluma ya kutosha kwenye kazi anayoenda kuifanya wakati huo huo wapo watu wenye ujuzi mkubwa wa kufanya kazi hiyo.
     
    Dhambi hii ipo kwenye kila sekta nchini.Hivi juzi tu tumetoka kusikia kusitishwa kwa ajira za uhamiaji kutokana na mambo haya haya.Nchi yetu aiendelei kutokana na kukosa watu sahihi wakutuongoza,Baba Mwanaasha anaweza kuwa na mipango mizuri juu ya nchi yetu lakini watu wanaomzunguka wakawa wanamkwamisha. Nikijiuliza kwanini michezo yetu aiendelei nikagundua tatizo ni hili hill.Tumekosa watu sahihi wa kuongoza michezo yetu.Si riadha wala mpira wa mikono,mambo ndo yale yale kila siku tumekuwa watu wa kushindwa.Huku kwenye mpira wa miguu ndio kabisaa kila siku afadhali ya Jana.
     
    Anko anaweza akawa na maono mema na soka letu lakini tatizo likawa kwa watu aliowaweka karibu.Sijui wanamshauri nini anko watu hawa?.Anko watu hawa ndio wanakukwamisha na kukwamisha soka letu kwa ujumla.Sawa anko, najua ufanyi kazi peke yako ila nakulaumu kwa kukimbia kitu kinachoitwa 'scale of preference'.Anko umenifanya nimkumbuke mzee Johnson Mbwambwo,Mzee Johnson Mbwambwo ambaye ni muandishi mashuhuri wa habari za siasa alishawai sema maneno haya"Watawala wengi Duniani hasa wa nchi zetu za Afrika wanapenda mno kuzungukwa na watu (walamba miguu) ambao unaweza kuwaita court jesters au hata sycophants.

    Kwa kawaida watu hawa kazi yao ni kusifia kila kitu rais  anachokifanya au kukitamka,na wanafanya hivo ili wampendezeshe na aone kuwa watu wanampenda.Rais akicheka wao watacheka zaidi,Rais akinuna wao wananuna zaidi,Rais akimkasirikia mtu wao humkasirikia mtu huyo zaidi.Rais akitukana wao hutukana zaidi.Ni Court jesters hao ambao kihulka unaweza kuwaita Sycophants.”

    Anko nahisi kuna court jesters wanakutafuna na kukurudisha nyuma.Anko ungekuwa na washauri wazuri tusingekua tunahesabu siku zetu za nyuma.Anko leo mnapanga hiki kesho mnatengua si utoto huo.Anko leo nataka nikueleze mambo mawili kati ya mengi niliyonayo ambayo walibidi wafanye washauri wako wa karibu ambao ni viongozi wenzako wa shirikisho.

    La kwanza ni hilo nililoanza kuligusia hapo juu.Anko awali mliweka agosti 3 kuwa mwisho wa usajili mkasogeza mbele mpaka agosti 17,mkaona haitoshi mkaongeza tena siku na mpaka ukafika mwezi september.Anko hapa napata wasi wasi mkubwa na watu wanaokuzunguka.Huu uswahili mpaka lini?kwanini kila siku sisi tu? Kama tumeshindwa kusimamia jambo hili dogo tutaweza kweli kusimamia mashindano makubwa unayoyaota ukiwa macho?

    Anko kubwa na la msingi tulitarajia utatengeneza shirikisho jipya lisilo na chembe ya ukanjanja lakini majanga ni yale yale tena yanaendelea kuzidi.Anko nilitarajia shirikisho lako litajitenga na siasa za simba na yanga lakini haipo hivyo.Miaka michache iliyopita tulishuhudia usajili wenye utata wa Athuman iddi ‘chuji’,Kelvin yondani na Mbuyu twite na sasa Emmanuel okwi.Kanuni za usajili zipo lakini hazifuatwi.Hapa ndipo napata wasi wasi mkubwa na watendaji wa tff,Kuna kipindi kanuni ziliwekwa pembeni na mchezaji akaamuliwa acheze timu fulani kwa kupiga kura.Hii inatokea Tanzania tu.Anko mtazibeba simba na yanga mpaka lini?kwanini kila siku ni wao tu?.Au shirikisho letu halina kanuni zake bali linaongozwa na kanuni za simba na yanga? 

     Anko hao jamaa mbakushoborola batai?(wanakushauri nini).Ancle labda nikiuliza kwa lugha hii utajua nimemaanisha.Labda na hao jamaa wataelewa nnachozungumza.Anko bado una muda mwingi pia unao muda wa kufanya mabadiliko ya jamaa zako bila kujali ni rafiki au ndugu zako,kuna watu wa mpira wengi sana wanaweza kurekebisha madudu wanayofanya washauri wako wa sasa.Anko fanya hima watanzania wamechoka kusubiri.Usipofanya mabadiliko wataomba kukubadilisha.

                                                                      Na
                                                             


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIVI ANKO HAO JAMAA MBAKUSHOBOROLA BATAI? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top