Habari na Paul Manjale
Klabu ya Chelsea
inaonekana kunogewa zaidi na huduma za mlinda mlango wake raia wa Ubelgiji
Thibaut Courtois (22)baada ya hivi punde
kutangaza kuwa imemuongezea mkataba mpya wa miaka mitano nyota huyo.
Taarifa kutoka klabu ya
Chelsea imesema “Chelsea Football Klabu inayofuraha
kutangaza kuwa Thibaut Courtois amesaini mkataba mpya wa miaka mitano leo hii”
Courtois ambaye
alisajiliwa klabuni hapo mwaka 2011 akitokea klabu ya nyumbani kwao ya KRC Genk na kucheza kwa mkopo wa misimu mitatu
katika klabu ya Atletico Madrid ya
Hispania na kutwaa taji la La Liga amerejea Stamford blidge msimu huu na
kufanikiwa kumpora namba aliyekuwa mlinda mlango namba moja wa klabu hiyo kwa
muda mrefu Peter Cech (32).
Baada ya kusaini
mkataba huu Courtois alikuwa na haya ya kusema “Nimefurahi
kusaini mkataba huu mpya wa miaka
mitano.Ni furaha pia kujua kuwa nitaendelea kuwa hapa kwa kipindi kingine
kirefu,kilichopo akilini mwangu kwa sasa ni kuendelea kuipigania timu hii.
0 comments:
Post a Comment