MAKALA YA LEO
Allen Kaijage
0655106767
kaijagejr@gmail.com
Miaka ya 1950 alikuwepo dereva mmoja mmarekani
aitwae Blake.Blake alikua ni dereva wa mabasi ya abiria.Siku moja jioni wakati
akiendesha gari lake aligundua kuna abiria wapatao watatu ambao ni wamarekani
weupe wamesimama wakati huo huo kuna wamarekani weusi wamekalia siti.Blake
aliamua kusimamisha gari na kuwaamuru wale watu weusi kusimama na kuwapisha
watu weupe wakae.Baadhi yao wakatii amri ya blake lakini kuna mdada mmoja
jasiri aligoma kusimama kuwapisha watu weupe wakae.Mdada huyo alijulikana kwa
jina la Rosa Parks. Rosa ni mmoja wa watu waliokua mstari wa mbele kupigania
uhuru wa watu weusi pamoja na Martin Luther jr.Blake alimtahadharisha Rosa
asipokubali kusimama atawapigia simu polisi wamkamate.Rosa bado aliendelea
kuweka mgomo na hapo ndipo Blake akawapigia simu polisi na Polisi wakaja
kumkamata Rosa kwa kosa la ukaidi.Mpaka leo watu weusi bado wanamkumbuka Rosa..
Stori hii ya luther haitofautiani na stori ya
Wacatalonia.Kule nchini Spain hakuna watu wabaguzi kama Wacatalonia.Wao wanapenda
vya kwao tu.Ubaguzi wao unawapeleka mpaka kuwaza kujitenga na Spain na
Catalonia iwe nchi huru.Katiaka kitongoji kimoja cha Catalonia kiitwacho
Santpedor ndipo alipozaliwa Pep Guardiola.Pep Guardiola kama Wacatalonia
wengine nae ni mbaguzi kweli kweli.Pep guardiola alipojiunga na Barcelona kitu
cha kwanza alichofikiria ni nafasi za Wacatalonia ndani ya timu ya
Barcelona.Pep kila akiwaangalia Henry,Etoo ,Yaya Toure na Deco wakiwa kwenye
kikosi cha kwanza cha Barcelona alikua hajisikii vizuri.Ukiangalia Wachezaji
hao wote hawajazaliwa Catalonia pia baadhi wana
asili ya ngozi nyeusi.Kitendo kile kilikua kinamuumiza sana
Guardiola.Guardiola akatafuta kila mbinu kuhakikisha wachezaji hao hawakipigi
Barcelona na nafasi zao zinachukuliwa na Wacatalonia.Henry kisa chake kilikua
pedro,Etoo akapewa Borjan, Yaya Toure akategwa kwa Sergio Bousquet na Deco
akanasa kwa Xavi.Guardiola alifanya maamuzi magumu kwa ajili ya kuinusuru
Catalonia yake.Kitendo cha Guardiola kuanza kuwasugulisha benchi
Henry,Etoo,Deco na Yaya Toure akitofautiani sana na kitendo cha Blake kuwaamuru
watu weusi wasimame kuwapisha watu weupe wakae kwenye siti.Henry kwenye kiwango
chake,Yaya kwenye ubora wake walikubali kuwapisha kirahisi Bosquet na Pedro
wachukue nafasi zao.Watu wengi hawakumuelewa Pep.Ila mwisho wa siku Wacatalonia
wenzake hawakumuangusha na kuifanya Barcelona ya Pep iliyojaa wazawa wengi kuwa
Barcelona bora kuwai kutokea.Pia Pep mpaka leo atakumbukwa kwa kutoa wachezaji
saba wa kikosi cha kwanza cha Spain kilichomfunga Uholanzi kwenye fainali ya
Kombe la Dunia mwaka 2010.Kwa ufupi Pep ndie alichangia kwa kiasi kikubwa
mafanikio ya timu ya taifa ya Spain katika kombe la Dunia mwaka 2010.
Kila nikitafakari Dhambi ya Guardiola naona
faida ndani yake.Guardiola amenifanya kuhisi kuna dhambi nyingine ni tamu kwa
wanaoifanya.Nawaza tu jinsi gani Tanzania tutafanikiwa tukiwa na Roho kama ya
Wacatalonia.Ukiangalia ligi yetu tumekuwa tukiwatukuza sana wachezaji wa
kigeni.Si wachezaji tu pia tumekuwa walamba miguu ya makocha wa
kigeni.Najiuliza kama Wacatalonia wasingeamua kumpa kibarua mtoto wa nyumbani
pep kama Barcelona na Spain wangetisha
vile?.Hapa bado nafikiria ingekuaje kama Kenny Mwaisabula angekua kocha wa
Yanga,Seleman Matola kocha wa simba na Kali Ongala angekua kocha wa Azam.Nahisi
mwaisabula nafasi ya Jaja angekuwa anampanga Bahanuzi au Tegete,Nafasi ya
Niyonzima angekua anacheza Dilunga,Pia angekua anampa sana nafasi Msuva na
ngasa kuliko Coutinho.Vivo hivyo kwa Selaman Matola,Mtola asingemfikiria Okwi
kuliko singano na Chanongo,Asingekua na haja ya kumpapatikia Kwizera wakati
yupo mtoto wa nyumbani Jonas Mkude,Pia ingekua rahisi kwa Maguli kupata nafasi
mbele ya Kiongera.
Lakini Maximo na Phiri hawawezi kufikiria kama
Mwaisabula na Matola wanavyofikiria.Maximo na Phiri hawana uchungu na
Tanzania.Damu nzito kuliko maji bwana .Matola na Mwaisabula wana uchungu sana
na Taifa lao.Wanaumia kama mimi wakiona Tanzania inavyoyumba kisoka.Lakini hata
siku moja usitarajie Maximo na Phiri watakua na maumivu hayo.Maximo ataendelea
kuwapa kipaumbele ndugu zake Jaja na Coutinho huku na sisi tukiendelea
kuwashangalia huku tukiwa tumesahau kuwa vipaji vya Msuva ,Tegete na Bahanuzi
vinaenda kuteketea.Phiri nae kama kawaida ataendelea kuwapa kipaumbele akina
okwi,Kiongera,Kwizera na Tambwe,wakati huo huo Jonas Mkude,Singano na Chanongo
wakiendelea kusugua benchi jambo linalohatarisha vipaji vyao.
Wengi
watakuja juu na kuniambia kama jaja anajua kuliko tegete kwanini asipangwe?
Nami ntakuuliza je wewe ulikua unaamini kama Pedro ni bora kuliko Henry?,Xavi
ni zaidi ya Deco?,Messi ni zaidi ya Ronaldinho?,Bosquet ni zaidi ya Yaya
Toure?.Wote tulikua hatuamini lakini kocha mzawa Guardiola alituaminisha na
wote tukaamini na kukubali.Pia mimi bado
naamini Jaja si lolote kwa Bahanuzi na Tegete,Jonas mkude ana ubora zaidi ya
kwizera kama kocha tu akiwaamini,Tatizo lililopo ni ngumu makocha wa kigeni
kuwaamini wachezaji wetu kuliko wachezaji kutoka nje ya nchi.
Kwangu
huu ni wakati sahihi kwa timu kubwa za Simba,Yanga,na Azam kujivika roho za
Wacatalonia kwa kuwaamini makocha wazawa
Kama Wacatalonia walivyomuamini Pep Guardiola.Naamini ni makocha wazawa tu ndio
wataliokoa soka letu kwa kulinda na kuendeleza vipaji vya wachezaji wetu.Wakina
Matola,Mwaisabula na Kibaden ndio watakaoistiri Tanzania yetu kama Guardiola
alivyofanya kwa Wacatalonia.
GUADIOLA ALIKUTA KIKOSI CHA FRANK RKAD,YEYE ALIFANYA MACHACHE TU GARI LIKAWAKA,NI DHAMBI KUMUANGUSHIA SIFA ZOTE YEYE WAKATI ALIKUTA MWENZIE KAMTENGENEZEA WATU ALIPOONA WANACHOKA AKAWAKIMBIA,KIPIMO CHAKE KIZURI NI BAYERN NGOJA TUONE ATAFIKA NAO WAPI MAANA LAST YR UKITOA BUNDESILIGA ALIVURUNDA CHAMPIONS LG NA KULE KWINGINE
ReplyDelete