Javier Hernandez
Chicharito ameitupia dongo klabu yake mama ya Manchester United na kudai kuwa
haikumuamini kabisa katika misimu miwili iliopita.
Chicharito (26) raia wa
Mexico ndani ya misimu miwili iliyopita alifanikiwa kuanza michezo isiyozidi
kumi (10) kikosi cha kwanza akifanya mahojiano jana baada ya kuiwezesha klabu
yake ya Real Madrid anayoichezea kwa mkopo kuibuka na ushindi mkubwa wa bao 8-2
dhidi ya klabu ya Derpotivo la Coruna alisema..
“ Hakukuwa na
imani.Ilinibidi kuwa na subira na ndiyo maana leo niko hapa.Msimu uliopita
ulikuwa ni mgumu sana kwangu sababu sikuaminika.”
Nilipata kukutana na
{Carlo} Ancelotti wakati ule akiifundisha Chelsea.Imani aliyonayo kwa wachezaji
wake imeniamsha na kunifanya nijitume zaidi”
“Nataka kuutumia vizuri
muda wangu wa kuwa hapa.Kila mchezaji anaota kuchezea Real Madrid.Najua niko
hapa kwa sababu.Takwimu zinanibeba,mimi ni mchezaji mzuri nan i mtu wa watu”alimaliza
Chicharito ambaye jana alianza kufungua akaunti yake ya magoli kwa kuifungia
Real Madrid goli mbili baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Gareth Bale.
0 comments:
Post a Comment