Habari na Paul Manjale
Wakati kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Mdachi Louis
Van Gaal akiwataka wachezaji wake wote wanaongea kihispania kufanya kila
wawezalo kujua kiingereza ili waweze kuendana vizuri na mazingira ya klabuni
hapo kama mafunzo na mambo mengine hali ni tofauti kidogo kwa kiungo wa klabu
ya Manchester City Muingereza James Milner.
Milner ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wachache wa
kiingereza wanaopata nafasi ya kucheza kila juma klabuni hapo ameona kuwa dawa
ya kurahisisha mawasiliano kati yake na wachezaji wenzake hasa wale wanaotoka
Hispania na Amerika ya kusini ni kuamua kuiendea darasani lugha ya Kihispania.
Hayo yamewekwa bayana na mlinzi wa zamani wa klabu hiyo
aliyetimkia klabu ya Fiorentina (Fiola) ya Italia Micah Richards wakati
akifanya mahojiano na jarida la The Guardian.Richards amesema
Milner akiteta jambo mazoezini na David Silva hii ni mwaka 2011 |
“Kwa
miaka kadhaa sasa Milner amekuwa akijifunza Kispania ili aweze kuwasiliana na
akina Aguero,David Silva,Pablo Zabaleta,Martin Demichelis,Ruben Cousilas na
kocha Manuel Pellegrini.Nakumbuka kuna wakati nahodha Vincent Kompany aliwahi
kuwaambia wachezaji wote wanaoongea Kihispania wajifunze Kiingereza lakini bado
wamekuwa wazito kufanya hivyo”
0 comments:
Post a Comment