Paul Manjale
0717 70 55 48
Klabu ya Real Madrid iliyokuwa na nyota wao kibao wa bei
mbaya imekubali kichapo cha goli 4-2 toka kwa klabu ya Real Sociedad katika
mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Anoeta.
Madrid iliyokuwa bila ya nyota
wake Cristiano Ronaldo ndiyo iliyokuwa ya kwanza kutikisa nyavu za wenyeji
Sociedad baada ya kupata magoli ya haraka haraka kupitia kwa mlinzi Sergio
Ramos na winga Gareth Bale.Baada ya magoli hayo Sociedad walikuja juu na
kufanikiwa kurudisha goli moja baada ya jingine na kasha kuongeza kupitia
washambuliaji wake hatari wakiongozwa na David Zuruzuta(41,65),Inigo Martinez
(35) na Carlos Vela (75).
Katika mchezo mwingine wa La Liga klabu ya Barcelona
imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kuifunga timu ngumu ya Villareal kwa
goli 1-0 kupitia kwa kinda wake Sandro Ramirez (19) dakika ya 82 ya mchezo huo
uliopigwa katika dimba la El Madrigal.
Sandro akicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi cha
kwanza cha Barcelona aliingia dimbani kuchukua nafasi ya Pedro Rodriguez na
kufanikiwa kufunga bao hilo muhimu na la pekee kufuatia kazi nzuri iliyofanywa
na mchezaji bora wa zamani wa dunia Leonel Messi baada ya kuwazidi unjanja
walinzi viburi wa Villareal.
0 comments:
Post a Comment