Bundi ameendelea kutamba katika anga la klabu ya Manchester
United baada ya hapo jana klabu hiyo yenye masikani yake katika dimba la Old
Trafford kubamizwa goli 4-0 na klabu ya daraja la chini ya Mk Dons na hivyo
kuiaga michuano hiyo kwa msimu huu.
Huu ni mchezo wa tatu wa mashindano kwa United kucheza ikiwa
chini ya kocha mpya Mdachi Louis Van Gaal akiwa ameambulia sare moja tu na
kupoteza michezo miwili ndani ya wiki moja na nusu.
Hii ni mara ya pili kwa Klabu ya Manchester United kutolewa
katika mzunguko wa pili tangu ilipofanya hivyo mwaka 1995 pale ilipotupwa nje
ya michuano hiyo na klabu nyingine ya daraja la chini ya York City.
Dons ilipata magoli yake kupitia wachezaji wa mkopo Will
Grigg (kutoka Brentford) aliyefunga mara mbili huku kinda wa Arsenal aliyeko
klabuni hapo kwa mkopo Benik Afobe naye akifunga mara mbili mbele ya mashabiki
26,969 huku mfumo wa 3-5-2 ukionekana dhahiri kuwashinda walinzi wa Manchester United.
0 comments:
Post a Comment