Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Msenegal Demba Ba
amemtupia kombora kocha wake wa zamani katika klabu hiyo Mreno Jose Mourinho
akimtuhumu kuwa hakumpa nafasi ya kuonyesha kipaji chake na badala yake alitoa
nafasi kulingana na majina.

Ba akiongea na gazeti la The Sun amemlaumu kocha Jose
Mourinho kuwa yeye ndiye aliyekuwa kikwazo cha yeye kufanya vizuri katika klabu
hiyo kwa sababu alipendelea kuwatumia zaidi washambuliaji Samwel Eto’o na
Fernand Torres badala yake kwasababu ya majina yao.
Alisema “Kuna wakati unapokuwa kwenye klabu yenye nyota
wengi ,majina hupewa kipaumbele zaidi kuliko takwimu.Kwa bahati mbaya ilikuwa
hivyo kwa upande wangu.Nilipewa nafasi wakati
Eto’o na Torres hawakuwepo”alisema nyota huyo mwenye miaka 29.
“Lakini nina furaha nilihama kutoka Newcastle na kutua
Chelsea na nikapata nilichokipata.Nina marafiki wengi hapo.Eden Hazard ni
rafiki yangu mkubwa,niko karibu na Ivanovic pia.Nawatakia kila jema ili waibuke
na taji la ligi msimu huu.

JE ILIKUWAJE
AKASHINDWA KUTUA KWA MKOPO ARSENAL?
Wakati huohuo pia Demba Ba alichua kuwa alikuwa karibu kutua
Arsenalkwa mkopo lakini uhamisho huo
ulizimwa dakika za mwisho na kocha Jose Mourinho kwa kuwa hakutaka kutoa siraha
kwa mpinzani wake.

KUELEKEA MCHEZO WA
KUSAKA TIKETI YA LIGI YA MABINGWA DHIDI YA ARSENAL BA AMESEMA!!
Tumejiandaa vizuri dhidi ya Arsenal tunataka kushinda mechi
zote mbili na hatimaye kupata nafasi ya kucheza katika hatua ya makundi ya ligi
ya mabingwa.Kikosi chetu bado ni kichanga kina vijana wengi wanaotaka kujifunza
wanaoutaka mpira muda wote.Hatuna aina ya washambuliaji kama walioko Chelsea
lakini tutahakikisha tunawashinda Arsenal kama walivyofanywa pale Stamform
Bligde msimu uliopita kwa kichapo cha goli 6-0.
0 comments:
Post a Comment