Klabu ya Southampton baada ya kutawala sana soko la usajili
msimu huu kwa kuuza nyota wake mahiri sasa nayo imeanza kusajili ili kujipanga
upya baada ya kuridhika na mauzo iliyoyafanya.
Klabu hiyo inayotumia dimba la St Mary’s baada ya kumsajili
mshambuliaji Grazziano Pelle,Ryan Betrand na Dusan Tadic sasa imefanikiwa kumnasa kwa mkopo kiungo wa
klabu ya Inter Milan Mualgeria Saphir Taider 22 ambayo aliiwakilisha vyema timu
yake ya taifa katika michuano iliyoisha ya kombe la dunia.
Katika usajili huo imeshuhudiwa pia klabu hiyo ikikubali
kumtoakwa mkopo mshambuliaji wake Pablo
Osvaldo kwenda klabu ya Inter Milan huku kukiwa na makubaliano ya kufanyika
mabadilishano rasmi mwisho wa msimu.
0 comments:
Post a Comment