Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Crystal Palace Tony Pulis (
56) ameachana na klabu hiyo zikiwa zimebaki saa 48 kabla ligi ya Epl haijaanza kutimua vumbi jumamosi
hii.Pulis alijiunga na klabu hiyo novemba 2013 akichukua nafasi ya kocha
aliyetimuliwa Ian Holloway baada ya mwenendo mbaya katika ligi.
Tony Pulis anaondoka baada ya msuguano wa mara kwa mara na
uongozi wa klabu hiyo hasa mwenyekiti Steve Parish katika masuala mazima ya
usajili yaliyopelekea kuwakosa nyota kama Gylfi Sigurdsson na Steven Caulke.Mpaka
sasa Palace imeshawanasa nyota kama Chris Kettings na Brede Hangeland, Fraizer
Campbell na Martin Kell.
Pulis anakumbukwa kwa kuinusuru Palace kushuka daraja baada
ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Chelsea na sare ya bao 3-3 dhidi ya
klabu ya Liverpool kulikopelekea kocha huyo kutwaa tuzo ya LMAO (Kocha bora wa
msimu akifungana na kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers).Palace inabaki
mikononi mwa kocha wa muda Keith Parish
0 comments:
Post a Comment