728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 17, 2014

    YA MOYONI:VAN GAAL,WENGER BADO MNAHITAJIKA SOKONI

    Tathimini na Paul Manjale

    Baada ya miezi miwili na ushee hatimaye ligi yetu pendwa ya Epl imeanza kutimua vumbi lake hapo jana huku tukishuhudia kutawala kwa vichapo na sare kadha wa kadha.

    Katika michezo ya jana mechi zilizovuta hisia za mashabiki wengi ni ile ya ufunguzi iliyopigwa katika jiji la Manchester katika dimba la Old Trafford kati ya wenyeji Manchester United dhidi ya wageni Swansea City pamoja na ile iliyopigwa jijini London katika dimba la Emirates kati ya Arsenal na ndugu zao Crystal Palace.
    Kilichovuta hisia katika mechi hizi ni usajili mpya uliofanya na Arsenal wa nyota kama Alexis Chambers,Mathieu Debuchy na Calum Chambers,upande wa pili ni ujio wa kocha mpya Louis Van Gaal na mfumo wake wa 3-5-2.

    Kwa bahati nzuri nilipata wasaa mzuri sana wa kuitazama michezo hiyo miwili toka dakika ya kwanza mpaka ya mwisho huku nikiwa sijastushwa sana na matokea yaliyopatikana kwa kuwa vilabu vyote Arsenal na Manchester vimeanzia vilipoishia msimu uliotangulia.

    Nasema walipoishia kwa maana kuwa Arsenal wameendelea kupata ushindi finyu hasa kwa timu ambazo walipaswa wazishushie mvua ya magoli huku nao Manchester wakiendelea kuwasononesha mashabiki wao kama ilivyokuwa miezi kadhaa nyuma.Kipindi kile cha anguko la David Moyes ambaye mpaka leo bado analia kuwa hakupewa muda wa kutosha kujipanga.

    Nikianza na mchezo wa kwanza kati ya Manchester United na Swansea City magoli waliyofungwa Manchester yalitokana na counter attacks ambapo wabeki Chris Smalling,Phil Jones na kinda Blackett walizidiwa ujanja na hatimaye kushindwa kujipanga hivyo kutoa nafasi kwa Routridge,Bony,Ki na Sigurdsson kurikaribia na kulitia kashikashi lango la Manchester United.Safu hii ilionekana kukosa kiongozi na mtu mwenye uzoefu wa mfumo wa walinzi watatu.

    Katika kiungo Herrera na Fletcher bado wanahitaji kucheza zaidi ili wapate kuzoeana hii ilikuwa ikijidhihirisha sana kwani kuna wakati kulikuwa na umbali mrefu sana kati ya viungo hao hivyo ikawa rahisi kwa viungo wa Swansea wakiongozwa na Jonjo Shelvey,Ki na Dyre kuwa na uwanja mpana wa kukimbia,kupiga pasi na kumiliki mpira.

    Ushambuliaji bado ulionekana kuwa na kimya mno kwani Mata,Chicharito ni kama walipotea mchezoni huku Rooney na Januzaj wakionyesha matumaini kuwa iko siku watafanya kitu ikiwa tu atapatikana mtu/watu wa kuwafikishia mipira miguuni.Young na Nani majukumu yaliwazidi vimo,kushambulia na kurudi kuzuia ilikuwa ni mtihani kwao.

    Kwa upande wa Arsenal matatizo ni yale yale ya jana na juzi,safu ya ulinzi bado imeendelea kufungwa magoli ya mipira ya kutenga.Goli alilofunga mlinzi wa Crystal Palace Brede Hangeland ni kielelezo tosha kuwa bado Wenger ana Kazi kubwa sana ya kutibu gonjwa hilo ambalo limeendelea kumuadhibu siku hadi siku.Walinzi bado wanashindwa kujipanga vizuri na kuhakikisha mpira yote yenye madhara inaondoshwa langoni kwa ustadi na umahiri mkubwa.

    Safu ya kiungo cha ulinzi bado inamkosa mtu sahihi,mpambanaji na mwenye roho ngumu Arteta alipata shida sana kuzuia kashikashi za Chamakh.Huku ushambuliaji ukiwa bado tumeona jinsi ambavyo Wenger anapingana na ukweli na kutaka kujenga mazingira hatarishi ya kuwatumia Olivier Giroud na Yaya Sanogo kama washambuliaji wa kati.Sikumbuki mengi kuhusu Sanogo zaidi ya shuti moja tu ambalo alipiga nje......huyu kwangu jana ndiye alikuwa mchezaji mbovu zaidi.

    Muda bado upo wa kuyapatia ufumbuzi mapungufu yaliyojitokeza,ndiyo maana nikasema Van Gaal na Wenger bado wanahitajika sokoni.

     Hii ni wake up Call.......
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YA MOYONI:VAN GAAL,WENGER BADO MNAHITAJIKA SOKONI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top