KUTOKA THE MIRROR:Habari zinasema kwamba vilabu vya Tottenham na Psv vimefikia
makubaliano juu ya usajili wa winga mahiri wa Kidachi Memphis Depay.
Katika
makubaliano hayo ambayo awali ilidhaniwa kuwa Tottenham wangetoa kiasi cha Euro milioni 20 ili kumnasa nyota huyo
aliyetamba vilivyo akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi (The Orange)
katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
Katika makubaliano mapya klabu ya Tottenham imekubali kutoa
kitita cha paundi milioni 10 pamoja na nyota wake wa Kibelgiji Nacer Chadli.Chadli
aliyetua Tottenham msimu uliopita amejikuta akiwa nje ya mipango ya kocha mpya
Muagrentina Mauricio Pochettino.
0 comments:
Post a Comment