Baada ya kiungo wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez
kutangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa ya Hispania leo jumanne wachezaji
mbalimbali duniani wameshitushwa na uamuzi huo.Baadhi ya wachezaji hao ni
kiungo wa zamani wa klabu ya Arsenal Emanuel Frimpong,mlinda mlango wa klabu ya
Liverpool Pepe Reina,kiungo wa Arsenal Santi Cazorla na mshambuliaji wa klabu
ya Chelsea Fernando Torres.
Frimpong
amesema “Dunia imepoteza kiungo bora zaidi wa kati kuwahi kutokea”
Xavi mwenye umri wa miaka 34 alianza kuitumikia timu yake
ya taifa maarufu kama La Furia Roja mwaka 2000.Mpaka anastaafu Xavi amefanikiwa
kuichezea kokosi hicho jumla ya michezo
133 katika miaka 14 ya machozi,jasho na
damu.
Xavi anastaafu akiwa ameiwezesha Hispania kutwaa mataji
makubwa matatu ambayo ni kombe la dunia (2010) na mataji mawili ya Ulaya maarufu kama Euro
(2008 na 2012) huku mwaka 2008 akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano
hiyo.
Xavi anastaafu baada ya kushindwa kuivusha La Roja
kuingia japo hatua ya makundi katika fainali za dunia za mwaka huu zilizotimua
vumbi nchini Brazil na timu ya taifa ya Ujerumani kuibuka mabingwa.
@Paul Manjale
0 comments:
Post a Comment