Kocha mkuu wa klabu ya Besktas ya Uturuki Mcroatia Slaven
Bilic ameionya klabu ya Arsenal kuwa isitegemee kupata ushindi rahisi
itakapokutana na vijana wake katika mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza hatua ya
makundi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya utakaopigwa leo jijini Instanbul katika
dimba la Ataturk Olympic.
Bilic akitoa maelekezo dimbani |
Bilic ambaye ni kocha wa zamani wa vilabu vya Westham United
na Everton amesema “Hatuko hapa kupiga picha na wachezaji wa Arsenal uwanjani
bali tuko hapa kupambana mpaka dakika ya mwisho.Usitegemee kuona wachezaji wetu
wakipiga picha na Alexis Sanchez,Olivier Giroud ama Mikel Arteta or wakigombea
jezi za Arsenal wakati wa mapumziko,tunaamini tunaweza kufuzu na tutafanya kila
njia kuhakikisha hilo linafanikiwa.
Slaven Bilic akivuta sigara baada ya mechi |
Tunawajua wapinzani wetu vizuri na wengi wanawapigia chapuo
kufuzu lakini hii haituzuii kupambana na hatimaye kuwatupa nje ya michuano ya
Ulaya.
Itazame nembo ya ligi ya mabingwa nyuma yangu,wanasema picha
inaongea maneno elfu.Itazame nembo hiyo,hapo ndipo tunapopataka,huo ndiyo
mpango wetu na hiyo ndiyo ndoto yetu” Alimaliza Bilic
Katika mchezo huo klabu ya Arsenal itamkosa mlinzi wake wa
kushoto Kierran Gibbs na mshambuliaji Yaya Sanogo ambao wote ni majeruhi huku
Laurent Koscienly akisafiri na timu licha ya kuwa majeruhi wa misuli.
0 comments:
Post a Comment