Kwa mujibu wa neno la kanisa hili,soka ni dini na kama
ilivyo kwa dini yoyote ile kuwa na Mungu.Mungu wa soka ni Muargentina na jina
lake ni Diego Armando MaradonaDini hii ilianzishwa tarehe 30 0ctober 1998 huko Rosario,Argentina
na wafuasi wa Maradona ambao wanaamini
yeye ndiye mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea .
Mpaka leo dini hii ina wafuasi zaidi ya 100,000 katika nchi
zaidi ya 55 duniani kote.Baadhi ya majina machache maarufu yaliyo na uhusiano
wa moja kwa moja na kanisa/dini hiyo ni pamoja na Gary
Lineker,Ronaldinho,Mauricio Pochettino(Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs).
Waasisi wa dini hii ni Hernan Amez,Alejandro na Hector
Campomar ambapo hutumia autography/historia ya maisha ya Maradona badala ya
Biblia
Mapri wa kanisa |
Muumini akisujudu |
Ndani ya kanisa |
AMRI KUMI ZA KANISA/DINI HIYO
1.
Mpira usitiwe doa/alama/uchafu kama D10S
alivyoagiza
2.
Penda soka kuliko vitu vingine
3.
Onyesha/tangaza mapenzi yako ya dhati katika
mchezo wa soka
4.
Zitetee rangi za Argentina
5.
Yatangaze maneno ya Diego Maradona pande zote za
dunia
6.
Abudu kwenye hekalu alilohubiria/fundishia
7.
Usilitaje bure jina la Diego Maradona katika
jina la klabu moja
8.
Shika mafundisho ya kanisa la Maradona
9.
Fanya jina la Diego liwe jina lako la pili
pamoja na la watoto wako
10.
No ser cabeza de termo y que no se te escape la Tortuga (Usiwe mkaidi/kibuli na usiache hua/mdhaifu
akutoroke)
JE,D10S NI
NINI?
Dios-Ni
jina la Kihispania likimaanisha Mungu
10 - Namba ya jezi ya Maradona
SALA “Diego wetu uliye kiwanjani,mkono wako wa
kushoto utukuzwe,
tuletee maajabu yako.Fanya magoli yako
yakumbukwe duniani mpaka mbinguni,
tufanyie
miujizayako kila siku,
wasamehe
waingereza kama sisi tulivyowasamehe Mafia/Wahuni wa
Napoli,
Usiache
ukamatwe Offside na utuokoe kutoka kwa Joao Havelange na Pele.Diego
Argentina kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1986
.
Katika
sikukuu hiyo Hernan Amez,Alejandro na Hector Campomar huvaa majoho/kanzu meupe
huku wakiwa wameshikilia mpira na taji la miba miba.
October 30 ni kimbukumbu ya kuzaliwa kwa maradona ambapo
kila ifikapo tarehe hii huadhimishwa sikukuu kubwa ikiambatana na
Misa,Ubatizo,Harusi na shamra shamra mbali mbali.................itaendelea
0 comments:
Post a Comment