Mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Arsenal Muhispania
Manuel Almunia (37) amelazimika kustaafu soka baada ya kubainika kuwa ana
matatizo katika moyo wake.
Almunia ambaye aliichezea klabu ya Arsenal kwa misimu
minane kabla ya kutua katika klabu ya Watford misimu miwili iliyopita
amebainika kuwa na tatizo hilo baada ya kushindwa mara tatu kufuzu vipimo vya
afya katika klabu ya Cagliari iliyokuwa tayari kumsajili katika dirisha hili
usajili barani Ulaya.
Almunia ambaye pia ni mlinda mlango wa zamani wa klabu ya
Celta De Vigo ya Hispania anatundika gloves zake baada ya miaka ishirini ya
kucheza soka la kulipwa katika nchi za Hispania na England huku mafanikio yake
pekee yakiwa ni kucheza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa wa Ulaya kati ya
Barcelona na Arsenal mwaka 2006 ambapo Arsenal ililala kwa goli 2-1.
0 comments:
Post a Comment