Baada ya habari mbaya za kipigo na kosa kosa za hapa na pale
katika usajili hatimaye nyuso za furaha zimeanza kuonekana katika klabu ya
Manchester United baada ya mlinzi Marcos Rojo (24) kutegemewa kusaini leo
kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa ligi ya Epl.
Marcos Rojo ambaye ni mlinzi wa kushoto wa kutumainiwa wa
klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno na timu ya taifa ya Argentina anatarajiwa
kuwasili leo makao makuu ya klabu ya Manchester United tayari kwa vipimo vya
afya na kusaini mkataba wa miaka mine wenye kipengele cha kuongeza mmoja
zaidi.Inaaminika Manchester United italazimika kutoa kitita cha paundi milioni
16 pamoja na winga wake mahiri wa Kireno Louis Nani kwa mkopo wa msimu mmoja.
Louis Nani anatazamiwa kutua jijini Lisbon leo jumanne au
kesho jumatano kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kumwaga wino kwa mara
nyingine tena kuichezea klabu yake hiyo ya zamani kwa mkopo wenye kipengere cha
kuwa wa kudumu baada ya msimu huu wa 2014-2015.
Rojo ambaye wiki moja iliyopita aliingia matatani na
kutishiwa kuadhibiwa na klabu yake baada ya kugomea mchezo wa kirafiki pamoja
na mazoezi akishinikiza kuondoka klabuni hapo na kutua Manchester United
kutimiza ndoto yake ya tangu utotoni.
Usajili wa Rojo United unakuja wakati muafaka kwani klabu
hiyo kwa muda wa mwezi mmoja itazikosa huduma za mlinzi wake aliyemajeruhi Luke
Shaw hali iliyopelekea klabu hiyo kumtumia kinda Blackett katika mchezo wa
ufunguzi wa ligi na kuambulia kipigo toka kwa klabu ya Swansea City ya Wales.
Rojo pia ni tiba nyingine katika mfumo mpya wa 3-5-2 wa
kocha Louis Van Gaal kwani licha ya kuwa mahiri sehemu ya ulinzi wa kushoto pia
Muargentina huyo ni hodari achezapo kama mlinzi wa kati.
JE,NANI ANAHUSIKA KUMSHAWISHI ROJO ATUE UNITED?
Rojo akifanya mahojiano na kituo cha redio cha nyumbani kwao
kiitwacho Continental mapema jana alisema “Nimevutiwa na Manchester United
tangu kitambo sana nakumbuka Juan Sebastian Veron nikicheza nae katika klabu ya
Estudiantes aliniambia mengi sana kuhusu klabu hiyo”
0 comments:
Post a Comment