Habari na Paul Manjale
Kiungo wa klabu ya Arsenal Aaron Ramsey amewaomba radhi
mashabiki wa klabu hiyo baada ya kupata kadi nyekundu juzi katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu
kuingia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Ramsey akiwa na moja kati ya tuzo zake alizonyakuwa msimu uliopita baada ya kuibuka mchezaji bora wa mwezi |
Ramsey amesema “Asanteni mashabiki wote mliosafiri mpaka
Uturuki kuja kutuunga mkono lakini samahani sana kwa kadi nyekundu niliyoipata
katika mchezo huo.Natumaini wenzangu watashinda mchezo wa marudiano”.
Ramsey akitoka nje baada ya kupewa kadi nyekundu |
Ramsey alitolewa uwanjani dakika ya 80 ya mchezo baada ya
kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kosa la kumdondosha chini kwa kumvuta jezi
nyota wa klabu ya Besiktas na kinda wa zamani wa klabu ya Arsenal Ozyikup.
Ramsey atalazimika kuwa mtazamaji katika mchezo wa marudiano
utakaopigwa katika uwanja wa nyumbani wa klabu yake ya Arsenal wa Emirates
jijini London wiki ijayo ambapo mshindi wa mchezo huo atakata tiketi ya kuingia
katika droo ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment