Safari hii ile derby ya North-East ya mahasimu wakubwa wa
ligi ya Epl kati ya Manchesterb United na Liverpool inaanzia Marekani.Hii ni
baada ya vilabu hivi wiwili kushinda michezo yao ya jana usiku katika kinyang’anyiro
cha kombe la International Champions Cup.
Manchester United jana usiku iliwabomoa mabingwa wa Ulaya
klabu ya Real Madrid kwa jumla ya magoli 3-1 katika mchezo mkali uliokuwa na
vuta ni kuvute katika vipindi vyote viwili huku vijana wa Luis Van Gaal
wakionekana kuumudu vilivyo mfumo mpya wa 3-5-2.Katika mchezo huo magoli ya Manchester
United yalifungwa na Ashley Young aliyefunga mara mbili na Javier Hernandez “Chicharito”
alifunga mara moja huku lile la kufutia machozi la Real Madrid likifungwa na
winga Gareth Bale kwa mkwaju wa penati.
Liverpool nao hawakuwa nyuma kwani waliikimbiza watakavyo
klabu iliyobaki jina ya Ac Milan na kuishindilia jumla ya magoli 2-0 katika
mchezo uliofanyika katika dimba la Bank of America.Liverpool waliotumia mfumo
wa 4-3-3 walionekana kuizidi ujanja klabu ya Ac Milan tangu mwanzo wa mchezo
huo mpaka mwisho huku nyota wa mchezo huo akiwa ni kinda wa klabu hiyo Jordan Ibe.
Magoli yalifungwa na Joe Allen (16) na Suso (89)……………………Mchezo
wa fainali kati ya Liverpool na Manchester United utafanyika jumatatu jijini
Miami……….Je nani ataibuka mshindi?ni jambo la kusubiri na kuona…….
0 comments:
Post a Comment