Ndoto za kocha mkuu wa klabu ya
Arsenal Mfaransa Arsene Wenger kutotaka kusikia habari za kusajili mshambuliaji
mpya zimeingia mdudu baada ya mshambuliaji wake tegemeo Mfaransa Olivier Giroud kuhofiwa kuwa nje kwa kipindi cha miezi
mitatu baada ya kuumia kifundo cha mguu jumamosi iliyopita.
Giroud aliumia wakati akijaribu
kuzuia mpira uliopigwa na mlinzi wa Everton Sylvian Distin zikiwa ni dakika
chache tu tangu mshambuliaji huyo afungu goli za kusawazisha akitokea benchi
kuchukua nafasi ya Mchile Alexis Sanchez ambaye alianza kama mshambuliaji wa
kati.
Habari kutoka ndani ya klabu ya
Arsenal zinasema Giroud huenda akawa nje kwa kipindi cha karibu miezi mitatu
baada ya jeraha lake kuonekana kubwa kuliko ilivyodhaniwa hapo mwanzo.Taarifa
kamili za mwisho juu ya lini hasa nyota
huyo atakuwa nje ya dimba zitatolewa leo na madaktari bingwa wa klabu hiyo kwa
kuaqnzia nyota huyo atakosa mchezo wa jumatano wa kusaka tiketi ya ligi ya
mabingwa dhidi ya Besktas ya Uturuki.
Kutokana na kadhia hiyo kocha
Arsene Wenger atalazimika kuingia tena sokoni kusaka mshambuliaji mpya baada ya
hapo mwanzo kutokuwa na mpango huo huku
kukiwa na habari ya kuwa karibu kumuuza mshambuliaji wake Mjerumani Lukas
Podolski kwenda vilabu vya Juventus ama Wolsburg.
Kati ya majina yanayotajwa tajwa
kutua Emirates kuziba pengo la mshambuliaji Olivier Giroud ni pamoja na nyota
wa klabu ya Manchester United Danny Welbeck,Loic Remmy na nyota wa Torino
Alessio Cerci.
0 comments:
Post a Comment