Habari na Paul Manjale
Real Madrid?
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Barcelona Mruguayi Louis
Suares (27) ameapa kuwa hatokuja kumng’ata mpinzani wake na kukiri kuwa amekuwa
akipata msaada wa ushauri toka kwa mwanasaikolojia tangu alipozamisha meno yake
kwenye bega la mlinzi wa Italia Georgio Chiellini wakati wa fainali zilizoisha za
kombe la dunia nchini Brazil.
Suarez akikagua meno yake baada ya kumng'ata Chiellini |
Suarez ambaye hivi karibuni alipunguziwa adhabu na mahakama
ya michezo CAS na kuruhusiwa kufanya
mazoezi pamoja na kucheza mechi za kirafiki amesema
“Nawaambia mashabiki msiwe na shaka kwasababu sitorudia tena kitendo
kile.Nimeongea na mwanasaikolojia wangu na ameniambia dawa ni kukubali
kilichotokea na kuomba radhi.Tayari
nimeomba radhi na akili yangu kwasasa ni kuitumikia klabu yangu ya Barcelona.
Wakati huohuo Suarez ameelezea furaha yake baada ya kucheza
mechi yake ya kwanza akiwa na klabu ya Barcelona katika ushindi walioupata wa
goli 6-0 dhidi ya klabu bingwa ya Mexico Club Leon.Amesema
“Siyo kuwa kucheza tu bali
pia kuwa chumba kimoja cha kudalishia nguo na wachezaji kama Leonel Messi na
Neymar kunanifanya nijisikie furaha sana”Inakufanya ujisikie furaha na hamasa
kucheza npamoja nao.Sijioni kuwa nyota,nyota ziko angani.
Niko tayari kucheza
popote pale katika ushambuliaji.Nimecheza mechi nyingi nikitokea winga ya
kushoto au winga ya kulia nikiwa na Liverpool kwa sababu Daniel Sturridge
alikuwa akicheza namba 9.Hivyo sina tatizo kucheza nafasi yoyote ya
ushambuliaji atakayonipanga kocha.
Je,ni kweli aliikataa ofa ya
Real Madrid?
Suarez “Ndoto ya
kuchezea Barcelona inaanzia miaka mingi sana,tangu nikiwa motto.Kila mtu anajua
kwamba baadhi ya jamaa wa familia yangu wanaishi hapa.Kulikuwa na ofa toka
vilabu vingi lakini ilipokuja Barcelona sikujiuliwa mara mbili ilikuwa ni
kutimia tu ndoto”.
“Nimekuwa nikipenda
sana kuja Camp Nou nilikuwa hapa wakati Barcelona ikiifunga Madrid goli
5-0,Arsenal 4-1 na Espanyol 1-0 goli la Andres Iniesta”Alimaliza Suarez
0 comments:
Post a Comment