Moja kati ya maamuzi ambayo bado yanaitesa vilivyo klabu ta
Newcastle United ni hatua yake ya kukataa kutoa dau kiduchu na kumpata kiungo
Aaron Ramsey.
Habari iko hivi…..Neil Bartholomew (msaka vipaji wa klabu
hiyo) aliipasha habari klabu ya Newcastle juu ya kiungo mwenye kipaji kikubwa
cha soka nchini Wales akiwa na klabu ya Cardiff .Baada ya taarifa hizo klabu ya
Newcaster ilimtumia tiketi ya ndege Aaron Ramsey pamoja na wazazi wake kwa
ajili ya kuja kufanya majaribio klabuni hapo.
Baada ya majaribio ya mara kwa mara Newcastle wakaonekana
kuvutiwa na mchezaji huyo kinda aliyekuwa na miaka 15 tu lakini kama ujuavyo
usajili wa makinda kwa vilabu vingi huwa ni kama kucheza kamari tofauti na
mchezaji mkubwa Newcastle wakakataa kutoa kiasi cha paundi 500,000 tu kumnasa
Ramsey licha ya kuwa alikuwa na usongo sana wa kuichezea klabu hiyo.
Kama ujuavyo ya Mungu mengi,baada ya miaka miwili ya juhudi
na kujituma kwingi klabu ya Arsenal ilikuja na ofa nono kipindi kile ya paundi
milioni 5 na kumnasa kinda huyo ambaye leo ni staa kweli kweli katika dimba la
Emirates.
Ramsey akiwa na moj kati ya tuzo za mchezaji bora wa mwezi |
0 comments:
Post a Comment