Klabu ya Borussia Dortmund imeibamiza klabu ya Bayern Munich
goli 2-0 na kutwaa taji la Super Cup kwa
mara ya pili mfululizo kama ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi ya Bundesliga.Borussia Dortumund ikicheza mbele ya mashabiki wake
katika dimba lake la Signal Park Iduna mjini Frankfurt ilijipatia magoli yake kupitia
washambuliaji wake Henrikh Mkhitaryan aliyefunga
goli la kwanza dakika ya 23 na Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga goli la
pili dakika ya 62.
|
wachezaji wa dortmund wakisherekea kikombe cha super cup |
|
Aubameyang na Grotzesk wakishangilia ushindi |
|
wachezaji wa dortmund wakishangilia goli la kwanza |
Huu ni ubingwa wa pili mfululizo wa Super Cup kwa klabu ya
Borussia Dortmund baada ya kufanya hivyo mwaka jana kwa kuwafunga tena Bayern
Munich kwa jumla ya magoli 4-2.Kivutio katika mchezo huu alikuwa ni
mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang ambaye baada ya kufunga goli alivaa
kinyago cha Spider Man alichokuwa amekificha katika soksi zake muda wote wa
mchezo.
Katika mchezo huo Dortmund ilikuwa bila ya nyota wake Matt
Hummels,Marco Reus na Ilkay Gundogan wanaouguza majeraha wakati Bayern ilikuwa
bila ya nyota kama Frank Ribery aliye majeruhi,Arjen Robben na Basten
Schwanstiger walio mapumzikoni.
0 comments:
Post a Comment