728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 06, 2014

    UMEFIKA WAKATI WA KUACHA KUKUMBATIA UJINGA SASA NA KUKUBALI MABADILIKO.

    Makala na Abuu Hozza

    Mara ya mwisho kwa timu yetu ya taifa
    kushiriki michuano ya kimataifa ni zaidi ya
    miongo miwili iliyopita ambapo tulifuzu kwa
    fainali za mataifa ya Afrika kule Nigeria.


    Zaidi ya hapo tumekuwa na historia iliyojaa kufeli na
    kushindwa kwenye mpira wetu,TFF imekuwa
    ikiishi kwenye mipango mifupi ya voda fasta na
    kuacha kuwekeza katika mitazamo ambayo
    faida zake zinaweza kuwa za muda mrefu sana
    baadaye,mfano mpango wa kukusanya vipaji
    wa toka mikoani na wilayani wa hivi karibuni
    ambao umeshindwa kutoa matokeo yenye
    mwelekeo chanya.TFF kama watawala wa mpira
    wa nchi hii ni ajabu kutowashutumu ama
    kuwapongeza kwa matokeo yeyote ya timu yetu.
    Hapana shaka kwamba mpira wetu umekosa
    uelekeo,kitu kikubwa kinachoumiza ni kwamba
    tunaleta siasa na kufanya mpira ni kama sekta
    ya kilimo ambayo tumeshindwa kuwa na
    mipango imara na endelevu ya kilimo cha
    kisasa na kubaki kutegemea wakulima wa
    jembe la mkono walishe taifa zima huku
    tukijidanganya kwamba nchi yetu inainuka
    kiuchumi, hivyo basi sasa ni wakati wa kuanza
    upya na kuachana na ujinga uliotujaa vichwani
    mwetu na kuja na mfumo mpya kama taifa.
    Mfumo wa soka unaojali zaidi maslahi ya pesa
    kuliko hata mafanikio ya timu uwanjani
    hautatufikisha popote.


    Ni aibu kubwa mno kwa
    nchi kubwa kama hii yenye wakazi karibia
    milioni 44 kukosa wachezaji imara wasiozidi 30
    tu,wakiwa wameandaliwa vizuri kiakili,kiufundi
    na kiushindani ili kuweza kushinda katika ngazi
    ya juu na kuleta sifa kwa nchi yetu,kwa hilo
    hatuna kisingizo cha kuepuka uzembe wetu.
    TFF kama watawala wanajua kabisa mpira wetu
    haukui na uko taabani kimataifa hata mbele tu
    ya majirani zetu ambao kwa sasa wachezaji
    wao wengi wamejenga hulka ya kukimbilia hapa
    kwetu kwa ajili ya malisho bora yanayopatikana
    katika liki yetu.


    Lakini bado Shirikisho letusoka
    limejisahu na kutoa macho zaidi kwenye Ligi
    Kuu ya vilabu ya Vodacom kuliko hata soka la
    nchi hii ambalo ndio msingi mkubwa wa uwepo
    wake.TFF hawana budi kugeuka sasa na
    kuwekeza kwenye mfumo mzima wa soka letu
    hasa katika nyanja za soka la vijana,kuliko
    kuendelea kutilia mkazo Ligi kuu ambayo sasa
    ni taasisi huru inayoendeshwa na chombo
    chake binafsi.TFF wanapaswa sasa kukomaa
    hasa na mfumo wa mzima wa mpira wa nchi hii
    badala ya Ligi ambayo asilimia kubwa
    inaaendeshwa kwa maslahi ya wenye vilabu
    vyao. .
    Karibia kila taifa utakalolitaja lillofanikiwa
    kisoka limefanya juhudi za dhati na mipango
    imara,kiufupi ni mapinduzi ya kisoka kuanzia
    nchi za Afrika kama Ghana,Cape
    Verde,Algeria,Ethiopia na Nigeria, nchi za Ulaya
    kama kama Ujerumani,Ubelgiji,Craotia,Hispania
    na nchi kadhaa za Amarica kama
    Columbia,Costa Rica na Mexico kote wanafanya
    vizuri baada ya kuacha kukumbatia ujinga na
    kufanya mambo kisayansi. Bert Vogts akiwa
    mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka la
    Ujerumani,alitengeneza mabadiliko ya mfumo
    wa elimu ambao ulitoa nafasi ya kuibuliwa kwa
    vipaji vya soka la vijana,kupitia mpango wake
    huo shirikisho la soka la ujerumani lilisaidia
    kwa kutengeneza vituo bora 390 vya soka la
    vijana nchi ambavyo vyote vilikuwa vikongozwa
    na walimu waliofikia vigezo bora vya
    ufundishaji,leo hii Ujerumani ni nchi ambayo
    shule zake za mpira zinazalisha wachezaji
    vijana wengi zaidi kuliko hata mahitaji yao ya
    timu ya taifa na vilabu vyake.Mpaka sasa
    tayari wana vijana zaidi ya 40 ambao
    wamezaliwa mwaka 1995 na 1996 wenye
    namba za kudumu katika vilabu vikubwa
    vinavyocheza ligi ya Bundesliga.TFF hapa wana
    haja ya kutoa nafasi au hata kuajiri wataalamu
    waliobobea katika masuala ya kiufundi na
    mipango na sio kutoa nafasi kwa watu kwa
    kigezo cha kuwa mchezaji wa zamani au kocha
    mstaafu bila ya kuwa na mipango,elimu,upeo
    na utashi wa kutengeneza mfumo imara.
    Mpira wetu mpaka sasa sasa umekosa falsafa
    yake inayojulikana achilia mbali mipango ya
    muda mrefu,wakati leo hii kila mtu akiiga
    falsafa ya tik tak(mpira wa pasi fupi fupi na
    haraka) ya Hispania ,Wajerumani wao walikuwa
    wakiiboresha staili hii ili kupata yao.Fasalsafa
    Watanzania ya mpira haijulikani na wala
    hatujajua mpaka sasa kama tunahitaji kuwa
    nayo.Ni muhimu pia kuwa na falsafa yetu ya
    mpira ambayo itatatufanya na sisi tutambulike
    Afrika na hata dunia nzima ambayo hata
    wachezaji wetu watatengenezwa kupitia faslsafa
    hiyo.Kwa sasa kila mtu wazo lake ni kushiriki
    mashindano makubwa kama Mataifa ya Afrika
    au Kombe la Dunia lakini kila mmoja wetu
    kichwani mwake hana wazo la namna gani
    tunaweza kufika huko.


    Tunafanya mchakato kila
    siku wa kuendelea kushindwa badala ya kubuni
    imfumo itakayotupatia mafanikio.
    Tumekuwa magwiji wa kutafuta mchawi kila
    siku kama sio kocha basi jua jumba bovu
    litamwangukia mchezaji.Tulikuwa
    tukimlalamikia Samatta hafanyi vizuri akiwa
    timu ya taifa, akaja Kaseja tukalalama aachwe
    kiwango kimeisha,Ngassa nae kachuja,Chuji
    umri umeenda,Cannavaro hana akili ya mpira,
    sasa tunadai Yondani nae anatumia baadhi ya
    vitu.Tumechagua kukumbatia ujinga na
    kuukataa ukweli.Kubadili makocha wazungu
    kila siku haiwezi kuwa suluhisho
    ,na hii
    inanifanya niamini msemo wa kuwa,”ni ngumu
    kwa tabia za kale kufa haraka”.


    Wapo
    wanolalamika kuwa tuna tatizo la uwepo wa
    wachezaji wengi wa kigeni katika ligi yetu,Hii
    inazidi kutudanganya, hivi kwa Ramadhani
    Singano kucheza na Hamisi Tambwe
    hakumfanyi azidi kuwa bora?Domayo kucheza
    na Niyonzima hakumfanyi ajifunze mengi?
    Mbona hatulalamikii wingi wa makocha wa
    kigeni vilabu vyetu,au timu yetu ya taifa kuwa
    na utaratibu wa kufundishwa na makocha wa
    kigeni kila mara?Kuna wachezaji wengi sana wa
    kibongo katika katika ligi yetu wala hilo sio la
    kulalamika, sema tunachokosa ni wachezaji
    bora na wenye elimu bora ya mpira.


    Wataalamu wanasema inachukua karibia miaka
    kumi kumpata mchezaji aliyekamilia,na
    inachukua muda mrefu pia kupata kocha wa
    kiwango cha juu. Jim Hill aliwahi kusema,”
    mchezaji mpira hakuzaliwa ila mchezaji mpira
    anatengenezwa kama ilivyo pia kwa makocha”,
    hivyo kwa upande wangu tatizo la mpira wetu
    linaenda mbali zaidi, hasa kwenye mizizi ya
    soka letu na hapo swala kubwa na la kujiuliza
    ni vipi tunaweza kuwafunza vijana wetu?,kwa
    jinsi gani hasa tunaweza kuzalisha wanasoka
    bora ambao wanaweza kushindana katika level
    ya kimataifa?.Mifumo hii ya kuzalisha
    wanasoka vijana inahitaji kurutubishwa mara
    kwa mara,inahitaji uangalizi wa hali ya juu.Pia
    inahitaji kufanyiwa mabadiliko kila baada ya
    miaka michache kwakwa kuweka mawazo
    mapya na mbinu mpya bora na za kisasa za
    ufundishaji kwani mpira kila siku unabadilika
    na kuwa wa kisasa zaidi.Tanzania tumefeli
    kabisa kufanya hivyo kwa miongo kadhaa
    iliyopita.Mara kadhaa kweli tunakuwa tunapata
    wachezaji wazuri lakini mabadiliko ya muhimu
    kwenye mpira wetu bado hayajafanyika,mfumo
    wa kupata wachezaji wa timu zetu kwa kutumia
    mpira wa mtaani ni wa kizamani na haufanyi
    kazi katika ulimwengu wa sasa.Mpaka sasa
    umetufanya tuwe hatuna wachezaji
    waliotengenezwa kifundi,kielimu na hata namna
    ya kuishi kama wachezaji wa kulipwa na kufika
    viwango vya kimataifa.


    Umefika wakati sasa tuweke pembeni usanii
    wetu,siasa zetu na ubabaishaji katika mpira
    wetu wa bongo,zile danganya toto na mipango
    ya kupiga pesa ife,tuwekeze kwa ajili ya kizazi
    kijacho,mabdiliko hayo yazingatie na yawe
    alama na faslsafa mpya ya soka la taifa letu
    kuanzia ngazi ya taifa,makocha,wachezaji,na
    washabiki tukubali kwamba tunakwenda
    kubadili mfumo mzima wa soka la taifa letu
    mpira unakosa ubora wa kutosha na wala sio
    kwamba unakosa mafanikio ya
    kimataifa,tusahau can 2015,tusahau world cup
    2018,tusahau vilabu vyetu kushinda makombe
    ya kimataifa,hakuna mafanikio ya mzaha
    tutakayopata na hili tuache kudanganyana
    wenyewe.
    Wasalaaam.


    Mwandishi wa makalaa hii anajulikana kwa jina
    la Abuu Hozza unaweza kunipata kwa facebook
    au namba ya ya simu ya 0759422148 kwa
    maoni na ushauri.


    #Toa maoni yako#
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UMEFIKA WAKATI WA KUACHA KUKUMBATIA UJINGA SASA NA KUKUBALI MABADILIKO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top