Mshambuliaji mpya wa klabu ya Fc Barcelona Mruguayi Lous
Suarez leo atashuka dimbani kuichezea klabu hiyo mchezo wake wa kwanza baada ya
kupunguziwa adhabu na mahakama ya michezo CAS kwa kosa la kumng’ata mchezaji wa
Italia Gergio Chiellini katika fainali zilizopita za kombe la dunia.
Suarez akikagua meno yake baada ya kumng'ata Chiellini |
Suarez mazoezini |
Surez atakuwemo katika kikosi cha Barcelona kitakachovaana
na klabu bingwa ya Mexico Club Leon katika mchezo wa kirafiki wa kuwania taji
la Joan Gamper.Barcelona watautumia mchezo huo kuwatambulisha wachezaji wao
wapya kabla ya kuanza mshikemshike wa ligi ya La Liga dhidi ya klabu ya Elche
CF wikendi ijayo.
Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Suarez kuitumikia
Barcelona baada ya CAS kumruhusu kufanya mazoezi pamoja na kikosi hicho pamoja
na kucheza michezo ya kirafiki.
0 comments:
Post a Comment