Klabu ya Sunderland imefanikiwa kumsajili kiungo wa klabu ya
Manchester City Muingereza Jack Rodwell kwa mkataba wa miak mitano kwa ada
ambayo haikutajwa.
Rodwell anahama Manchester City ikiwa ni miaka miwili pekee
tangu atue klabuni hapo akitokea klabu ya Everton kwa ada ya paundi milioni 12.
Rodwell amefanikiwa kuichezea klabu hiyo jumla ya michezo 16
huku akiifungia magoli 2 yote yakiwa katika mchezo ambao Manchester City
ilifungwa goli 3-2 dhidi ya klabu ya Norwich City katika msimu wa 2012-2013.
0 comments:
Post a Comment