Klabu ya Manchester City iko katika mawindo ya kumsajili kwa mkopo wa miezi sita(6) kiungo wa zamani wa klabu ya Chelsea Muingereza Frank Lampard (36).Lampard ambaye hivi karibuni alikamilisha usajili katika klabu ya New York City inayoshiriki ligi ya MLS akiwa kama mchezaji huru baada ya kunyimwa mkataba mpya na klabu ya Chelsea ameonyesha kumvutia kocha wa City Manuel Pellegrini.
Pellegrini anaamini Lampard atakuwa na mchango mkubwa sana
hasa sehemu ya kiungo ya klabu hiyo ambayo imekuwa ikimtegemea zaidi kiungo
Muivory Coast Yaya Tourekatika kujenga mashambulizi
na nyakati nyingine kuzuia timu inapokuwa matatani.
Klabu ya New York City itaanza kukipiga MLS mwezi Machi
mwakani hivyo Manchester City inataka kutumia mwanya huo ili kumtumia Lampard
katika mechi za ligi kuu ya Epl pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya maarufu
kama Champions League.
Wakati huohuo kocha Manuel Pellegrini amesema kuwa klabu
yake haitofanya usajili mwingine zaidi mara itakapokuwa imemnasa mlinzi mahiri
wa klabu ya Porto Mfaransa Eliaquim Mangala.
@Paul Manjale
0 comments:
Post a Comment