Kiungo wa kimataifa wa England Frank Lampard 36 ametambulishwa kuwa
mchezaji mpya wa klabu ya New York City Fc itakayoshiriki ligi ya MLS
baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Lampard amepewa jezi namba 8 na kuwa mchezaji wa pili toka Ulaya
kusajiliwa na klabu hiyo baada ya mshambuliaji David Villa kufanya hivyo
mapema mwezi uliopita.
Usajili huo umehitimisha safari ndefu ya mafanikio ya Frank Lampard
akiwa na klabu ya Chelsea ambayo ameichezea jumla ya michezo 649 na
kuifungia magoli 241 huku akiwa amepika zaidi ya magoli 90 pamoja na
kutwaa mataji lukuki katika kipindi cha miaka 13 alichokuwa klabuni
hapo.
Lampard amesema licha ya yeye kuanza maisha mapya bado hafikirii
kustaafu kuichezea timu ya taifa kwani bado anaamini uwezo na nguvu
aliyonayo bado vinampa nafasi ya kucheza zaidiPosted by Paul Manjale
0 comments:
Post a Comment