Habari na Paul Manjale
Kocha mwenye maneno mengi ya karaha Mreno Jose Mourinho
amekitaka kikosi chake kujifunza kuzifunga timu zinazocheza mchezo wa kuzuia
zaidi maarufu kama kupaki basi ili yasijekuwakuta ya msimu uliopita hata
kufikia hatua ya kuukosa ubingwa wa ligi kuu.
Mourinho amekiri kwamba kikosi chake kiliteleza msimu
uliopita kutokana na kutokuwa na mbinu za kutosha kuzifunga timu zilizoingia
uwanjani kupaki basi alitolea mfano mchezo dhidi ya West ham ulioisha kwa sare
na kusema timu hiyo ilicheza soka la karne ya kumi na tisa (19).
Mourinho anaamini nyota wake wapya Cesc Fabregas na Diego
Costa watatatua tatizo hilo wakianzia na mchezo dhidi ya Burney usiku wa leo.
Mourinho amekiri kuwa kikosi chake kimefanya mazoezi mengi
katika kipindi cha maandalizi ya msimu (pre-season) kujaribu kuzifunga timu
zinazochezesha wachezaji kumi nyuma ya mpira(kupaki basi).
Mourinho amesema “Tunahitaji ubora katika mchezo wetu
,unapokuwa na mchezo wenye nafasi na muda ni rahisi kucheza mpira lakini
unapokuwa huna nafasi na muda ,unahitaji ubora zaidi na umahiri katika
umaliziaji.Tunalifanyia kazi hilo ili kuzizidi ujanja timu zinazoziba njia ya
kuelekea golini.
0 comments:
Post a Comment