Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal
Mfaransa Arsene Wenger anaamini
kuwa anaweza kupata vitu vingi kutoka kwa kiungo wake Aaron Ramsey kuliko alivyovipata kwa kiungo wake wa zamani
ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya Chelsea Mhispania Cesc Fabregas.
Wenger hakuweza kukwepa mkutano
na waandishi wa habari bila ya kuulizwa alijisikiaje baada ya kumuona kiungo wake wa zamani {Fabregas} akiwa amevaa jezi ya
klabu ya Chelsea ambao ni wapinzani wao toka jiji la London.
Kocha huyo alijibu “Jambo jema
katika maisha ni kwamba mtu anapoondoka mwingine anakuja na kupiga hatua.Rasmey
ana aina tofauti ya kiuchezaji ukimlinganisha na Fabregas ,lakini amepiga hatua
na kuwa mchezaji mmoja kati ya wachezaji nyota.Kuna mengi yanakuja toka
kwake.Bado ni mdogo ukimlinganisha na Fabregas na kuna matarajio ya kupata
mengi zaidi toka kwake.”
Pia Wenger anaamini kuwa Ramsey
atakuwa klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi na hivyo kuwa sehemu na kiungo cha
mafanikio kuliko ilivyokuwa kwa Fabregas ambaye aliondoka klabuni hapo katika
wakati ambao klabu ilihitaji zaidi huduma yake.
0 comments:
Post a Comment