Kocha mkuu wa klabu ya Atletico
Mdrid Muargentina Diego Simeone amefungiwa jumla ya michezo minane na chama cha
soka cha Hispania (RFEF) baada ya kutolewa nje katika mchezo wa pili wa kombe
la Spanish Super Cup ijumaa iliyopita dhidi ya wapinzani wao wa jadi klabu ya
Real Madrid.
Simeone alitolewa nje ya eneo la
kufundishia na mwamuzi David Fernandez Barbolan baada ya kulalamika mwamuzi wa
akiba alikuwa akichukua muda mrefu mno kumruhusu mlinzi wake Juanfran kurejea
uwanjani baada ya kufanyiwa matibabu yaliyotokana na kuumizwa na mchezaji wa
Real Madrid.
Kufuatia kitendo hicho kocha
Simeone alimgonga kwa mkono kisogoni mwamuzi wa akiba Antonio Santos Pargana wakati
akiondoka eneo la kazi la mwamuzi huyo.Pia kocha huyo mwenye vituko alipiga
makofi ambayo yanaaminika kuwa ni ya kejeri kwa mwamuzi huyo.
Simeone atakosa michezo miwili
kwa kosa la kulalamika,michezo minne kwa kumpiga mwamuzi wa akiba,mmoja kwa
kupiga makofi ya kejeri na mwingine dhidi kwa kosa la kutazama mechi kipindi
cha pili akiwa jukwaani.Kocha huyo pia amepigwa faini ya Euro 4,805 huku pia Atletico
ikiamliwa kutoa cha Euro 2,800.
RFEF pia imeshindwa kuchukua
hatua za kinidhamu dhidi ya Mreno Cristiano Ronaldo ambaye picha za televisheni
zilimuonyesha akimpiga mlinzi wa
Atletico Diego Godin dakika za mwisho za mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment