Michuano ya kombe la Emirates Cup inaanza leo kutimua vumbi lake jijini London katika dimba la Emirates ambapo miamba minne itavaana kusaka pointi tatu muhimu.
Miamba itakayoshuka dimbani leo jioni ni wenyeji wa michuano hiyo Arsenal,wageni Olympique Lyon,Wolfsburg na Villarreal.Michuano hiyo inatarajiwa kufikia tamati yake hapo kesho jumapili Julai 26 kwa timu yenye pointi nyingi zaidi ya nyingine kutwaa kikombe pamoja na zawadi.
Emirates Cup ambayo inadhaminiwa na shirika la ndege la Emirates ilianza mwaka 2007 na hushirikisha timu nne toka nchi mbalimbali na mechi huchezwa siku mbili tu.
Wakati huo huo kocha wa Arsenal,Arsene Wenger amesema mlinda mlango wa klabu hiyo Wojciech Szczesny hatokuwepo kwenye michuano hiyo kwakuwa uhamisho wake kwenda AS Roma kwa mkopo uko tayari na mkataba umeshaweka katika maandishi.Szczesny anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kati klabu ya AS Roma kabla ya kuitumikia miamba hiyo ya Seria A kwa mkopo wa msimu mmoja.
MECHI ZITAKUWA KAMA IFUATAVYO......
Jumamosi,Julai 25
16:00 VfL Wolfsburg v Villarreal
20:05 Arsenal v Olympique Lyonnais
Jumapili,Julai 26
Olympique Lyonnais v Villarreal
Arsenal v VfL Wolfsburg
0 comments:
Post a Comment