Katika tukio la ajabu Jumatatu ya jana, msanii wa vichekesho wa Uingereza, Lee Nelson alivamia mkutano wa Blatter na wanahabari, akasogelea pale Blatter alipokuwa amekaa na kujaribu kumkabidhi kitita cha noti za dola feki za Marekani.
Msanii huyo ambaye jinale halisi ni Simon Brodkin alimwambia Blatter: “Sepp, hizi (fedha zile feki) ni kwa ajili ya Korea Kaskazini 2026 (akimaanisha rushwa ili fainali za Kombe la Dunia 2026 zifanyike Korea Kusini).”
Ilibidi Blatter kuwaita walinzi wa Fifa kwa ajili ya kuingilia kati kumwondosha Nelson, lakini kabla ya kufanya hivyo alimmwagia Blatter noti hizo zikimpeperukia kichwani na kumzunguka huku Blatter akionesha kukasirishwa na kitendo hicho.
Blatter alinyanyuka kuondoka ukumbini na akapata salamu ya mwisho kutoka kwa Nelson aliyemwambia:
“Cheers, Sepp – zote (fedha) ziko hapo. Baada ya hapo wahusika waliziondoa noti hizo feki kisha baada ya dakika 10 Blatter akarejea kuendesha mkutano
0 comments:
Post a Comment