Kiungo nguli Xavi Hernandez amefichua kwamba Barcelona ilitaka abakie Nou Camp mpaka 2018 lakini yeye akachomoa na kuamua kujiunga na Al-Sadd ya Qatari mara baada ya mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Juventus.
Akiongea na kituo cha redio cha RAC1, Xavi 35 amesema: “Josep Maria Bartomeu alikuja nyumbani kwangu kunitaka nibaki Barca.Kabla ya hapo alishanishawishi pamoja na [Mkurugenzi wa zamani wa michezo Andoni] Zubizarreta na [kocha] Luis Enrique,wakitaka nibaki kwa mwaka mmoja zaidi.
“Kipindi hiki walikuja tena wakitaka nibakie mpaka 2018.Sikuwakubalia kwa kuwa niliona wakati wangu kuondoka umefika.Hivyo nikaondoka".
0 comments:
Post a Comment