Wojciech Szczesny akipiga picha na jezi atakayovaa katika klabu yake mpya ya AS Roma
Hatimaye mlinda mlango Wojciech Szczesny amejiunga rasmi na klabu ya AS Roma kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja akitokea katika
klabu ya Arsenal.
Wojciech Szczesny,25 ametua Roma baada ya kukosa uhakika wa namba katika klabu ya Arsenal hasa baada ya ujio wa mlinda mlango nguli Peter Cech toka klabu ya Chelsea ambaye ndiye atakayekuwa chaguo la kwanza huku David Ospina akiwa chaguo la pili.
Wakati mashabiki wengi wakijua kuwa uhamisho wa Wojciech Szczesny ni wa mkopo gazeti la The Mirror la England limekuja na habari kuwa huenda nyota huyo asiichezee tena Arsenal kwani AS Roma imepewa nafasi ya kumnunua mlinda mlango huyo kwa kitita cha paundi milioni tano mwishoni mwa msimu
Wojciech Szczesny akiwa na skafu ya AS Roma
Wojciech Szczesny akitazama picha za kikosi cha wachezaji wa AS Roma
0 comments:
Post a Comment