728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 24, 2015

    YANGA YAMRUHUSU SHERMAN AENDE AKASAKE MAISHA SAUZI

    Uongozi wa Yanga umetoa baraka kwa mshambuliaji wake, Kpah Sherman ambaye anatarajia kuondoka nchini kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya afya katika moja ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo kabla ya kukamilisha usajili.

    Sherman ameingia sokoni kutoka na uwezo wake kutolifurahisha benchi la ufundi la Yanga huku kukiwa na ushindani mkali wa namba ambapo washambuliaji wengine waliopo kikosini hapo Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Malimi Busungu.
    Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amesema kuwa, wapo katika mazungumzo ya mwisho na timu hiyo inayomhitaji Sherman.

    “Dili lipo katika hatua za mwisho na pindi litakapokuwa s ataondoka nchini kwa ajili ya kufanya vipimo na endapo atafu basi atajiunga na timu hiyo ambayo siwezi kukutajia jina lake sasa.

    “Hatupendi aende huko halafu akapate tabu ila tunatata akacheze soka, ndiyo maana hatukutaka aende kwa ajili majaribio kwani hiyo siyo hadh yake,” alisema Tiboroha.

    Aidha, mtu wa karibu wa Sherman amesema kuwa, Sherman ataondoka keshokutwa Jumapili au Jumatatu kujiunga na timu ya Mpumalanga Black Aces.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YAMRUHUSU SHERMAN AENDE AKASAKE MAISHA SAUZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top