Diaby:Klabu ya West Brom imeanza kumfukuzia kiungo wa zamani wa Arsenal Mfaransa Abou Diaby kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho. (Birmingham Mail)
Muller:Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema hakuna pesa duniani inayoweza kumnunua mshambuliaji wa klabu hiyo Thomas Muller.Kauli hii imekuja baada ya Manchester United kuripotiwa kuandaa kitita cha £70.5m kwa ajili ya kuinasa saini ya nyota huyo asiye na mambo mengi uwanjani.
Rolan:Kocha wa Aston Villa Tim Sherwood ameripotiwa kuanza kumfukuzia mshambuliaji wa Bordeaux Diego Rolan kama mbadala wa mshambuliaji aliyeondoka klabuni hapo Christian Benteke (Express & Star)
Ramos:Klabu ya Real Madrid inapambana kuhakikisha inambakisha mlinzi wake Sergio Ramos anayewindwa na Manchester United kutokana na kutokuwa na imani na afya ya mlinzi wake mwingine Raphael Varane.Kwa kipindi kirefu Varane amekuwa akisumbuliwa na tatizo la goti hivyo kufanya akose michezo mingi msimu uliopita hivyo Ramos hataruhusiwa kuhama. (El Confidencial)
Arsenal imeripotiwa kuwa tayari kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski ikiwa itashindwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema.(Metro)
Biglia:Klabu ya Lazio imeitupa ofa €25m toka klabu ya Manchester United kwa ajili ya kiungo wake Lucas Biglia kwa madai kuwa kitita hicho ni kidogo sana.Lakini klabu hiyo ya Italia imesema itamuuza Biglia ikiwa Manchester United itaongeza mpaka kufikia €40m.(Corriere dello Sport)
Otamendi:Klabu ya Valencia imesema haijapokea ofa yoyote kwa ajili ya mlinzi wake Nicolas Otamendi.Lakini Valencia imetanabaisha kuwa itakuwa tayari kumuuza Otamendi,27 ikiwa klabu yoyote kati zote zinazomtaka itakubali kutoa kitita cha €50m.(Superdeporte)
0 comments:
Post a Comment