Klabu ya Simba sasa mambo yao safi baada ya fedha Sh milioni 220 kuingia katika akaunti yao.
Fedha hizo ni malipo ya mauzo ya mshambuliaji Emmanuel Okwi Arnold kwenda katika klabu ya
Sonderjyske ya nchini nchini Denmark.
Sonderjyske ilikubali kulipa dola 110,000 ili kumnasa Okwi. Ikaahidi kulipa fedha hizo Juni 17 na imechelewa kidogo tu lakini imeweza kutimiza ilichoahidi.
Habari za uhakika kutoka Simba, zimeeleza kuwa Sonderjyske imeilipa Simba kupitia akaunti yake ya CRDB jijini Dar es Salaam.
“Kweli Simba wamelipwa fedha zao, lakini ni suala ambalo viongozi hawawezi kulizungumzia kwa sasa,” kilieleza chanzo.
Tayari Okwi yuko nchini Denmark katika kikosi chake cha Sonderjyske akiendelea kuitumikia timu yake.
0 comments:
Post a Comment