728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 24, 2015

    USAJILI:MOURINHO KUONGEZA MLINDA MLANGO MWINGINE DARAJINI,JORDAN AJEW NA JANNICK BOLASIE WAGEUKA DILI



    Diarra:Klabu ya Marseille imemsajili kiungo wa zamani wa vilabu ya Chelsea,Arsenal, Portsmouth na Real Madrid Lassana Diarra,30.Diarra amekuwa nnje ya dimba kwa kipindi kirefu baada ya kutemwa na klabu ya Lokomotiv Moscow ya Urusi.

    Ayew:Klabu ya Aston Villa huenda ikamsajili mshambuliaji Ghana Jordan Ayew baada ya klabu yake ya Lorient kuikubali ofa ya £12m.Ikiwa Ayew,23 atafanikiwa kutua Aston Villa atakuwa na kazi ngumu ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji Christian Benteke.(Sky sources)

    Bolasie:Vilabu vya Tottenham, West Ham na Aston Villa vimeanza kupigana vikumbo ili kuinasa saini ya winga msumbufu wa klabu ya Crystal Palace Mcongo Yannick Bolasie (Daily Mirror)

    Bettinelli:Klabu ya Chelsea iko tayari kutoa kitita cha £2.5m ili kumsajili mlinda mlango wa Fulham Marcus Bettinelli,23.

    Rahman:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kufikia makubaliano na klabu ya Ausburg kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Mghana Baba Rahman,21.Habari za ndani zinadai Chelsea itampa mlinzi huyo mkataba wa miaka mitano utakaomuwezesha kuvuna kitita cha £27,000 kama mshahara wa wiki.

    Diaby:Kiungo wa zamani wa Arsenal Abou Diaby,29 ameripotiwa kuwa katika makao makuu ya klabu ya West Bromwich Albion akifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya jiji la Birmingham.

    Digne:Klabu ya Liverpool huenda ikamsajili mlinzi wa kushoto wa klabu ya PSG Lukas Digne,22 baada ya nyota huyo Mfaransa kuuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa ataka kutua Anfield.(L'Equipe)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:MOURINHO KUONGEZA MLINDA MLANGO MWINGINE DARAJINI,JORDAN AJEW NA JANNICK BOLASIE WAGEUKA DILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top