Klabu ya Paris Saint Germain imekubali kumuuza mshambuliaji wake Mswedeni Zlatan Ibrahimovic kwenda katika klabu yake ya zamani ya AC Milan.
Kwa mujibu wa mtandao wa AlfredoPedulla.com,PSG wamekubali Ibrahimovic,35 arejee Milan mara baada ya mchezo wa Super cup utakaopigwa huko Montreal,Canada Agosti 1 dhidi ya klabu ya Lyon.
Habari za ndani toka kwa watu wa karibu wa Ibrahimovic ni kwamba tayari nyota huyo ameshakubaliana na AC Milan masuala yote binafsi ikiwemo mshahara wa €7.5m kwa mwaka mzima.
Ibrahimovic aliichezea Milan michezo 59 kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 42.
0 comments:
Post a Comment