Nguli wa soka Duniani ,Diego Maradona amemtuhumu mke wake wa zamani Claudia VillafaƱe kwamba kumuibia kiasi cha fedha zipatazo dola milioni tisa, katika akaunti yake ya benki.
Akizungumza katika matangazo ya moja kwa moja ya Luninga,Maradonna amesema VillafaƱe ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani ni mwizi. Hata hivyo VillafaƱe amepinga vikali madai na kudai kuwa yeye si
mwizi na hakuiba fedha hizo.
Wapenzi hao ambao walikutana katika mji uliokithiri kwa umasikini huko Buenos Aires kabla ya Maradonna kuwa maarufu na kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri duniani katika historia ya soka,waliachana kimapenzi kutokana na kutofautiana.
Watoto wao wawili Dalma and Giannina,wamekaririwa kwenye mtandao wa twitter wakimtetea mama yao wazi wazi na kwamba hahusiki na upotevu huo wa fedha za baba yao.
0 comments:
Post a Comment