Genk,Ubelgiji.
KLABU ya Genk inayochezewa na Mtanzania,Mbwana Samatta,imefuzu robo fainali ya michuano ya Europa Ligi licha ya leo usiku ikiwa nyumbani Luminus Arena kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na ndugu zao Gent kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.
Sare hiyo imeifanya Genk ifuzu robo fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-3 hii ni baada ya kushinda mabao 5-2 katika mchezo wa awali ulioshuhudiwa Samatta akifunga mabao mawili.
Katika mchezo wa leo Genk imepata bao lake kupitia kwa beki wake wa kushoto kutoka Ugiriki,Timothy Castagne katika dakika ya 20 huku Gent wakisawazisha katika dakika ya 84 kupitia kwa kinda wake Louis Verstraete na kuinyima Genk kupata ushindi wa nane wa Europa Ligi nyumbani.
Rekodi:Genk imeweka rekodi ya kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa Ligi huku pia Samatta akiweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kupata nafasi ya kucheza hatua hiyo.
Vikosi:
Racing Genk: Ryan - Brabec, Castagne,Colley, Uronen (81. Janssens) - Berge,Malinovsky, Pozuelo (46. Schrijvers) -Boëtius, Buffel (cap) (74. Trossard),Samatta
Kocha: Albert Stuivenberg (Ned)
AA Gent: Kalinic - Mitrovic (cap), Gigot, De Smet - Rabiu, Dejaegere, Foket, Simon -Kalu, Coulibalu, Perbet (62. Verstraete)
Kocha: Hein Vanhaezebrouck (Bel)
0 comments:
Post a Comment