728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 23, 2017

    Azam FC yaanza kuwawinda Yanga SC bila Bocco,Morris


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WAOKA MIKATE wa jiji la Dar Es Salaam,Azam FC leo wameanza mazoezi ya kujiandaa na mtanange wao wa Aprili 1 wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo,Yanga SC bila ya nyota wao wawili wa kutumainiwa mshambuliaji John Bocco pamoja na mlinzi Aggrey Morris. 

    Akizungumzia na Soka Extra msemaji wa Azam FC,Jaffar Idd Maganga amesema kukosekana kwa wachezaji hao kunatokana na kuendelea kusumbuliwa na majeruhi.

    Maganga amesema Morris anasumbuliwa na majeruhi ya misuli aliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland huku Bocco yeye akiwa nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu ya jeraha la goti ambalo limekuwa likimsumbua kwa kipindi kirefu sasa.

    Maganga ameongeza kuwa wachezaji wengine wote wa Azam FC tayari wameanza mazoezi isipokuwa wachezaji saba ambao wako kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kimeweka kambi jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi.

    Kwasasa Azam FC wako nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu bara wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza michezo 24.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Azam FC yaanza kuwawinda Yanga SC bila Bocco,Morris Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top