Rio de Janeiro,Brazil.
MLINZI wa Chelsea,David Luiz amesema kuwa ameumia baada ya kutojumuishwa kwa mara nyingine tena kwenye kikosi cha Brazil ambacho kimeweka kambi huko Rio de Janeiro, tayari kuzivaa Uruguay na Paraguay kwenye michezo miwili ya kimataifa ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia litakalofanyika mwaka 2018 huko nchini Urusi.
Luiz,30,hajawahi kujumuishwa kwenye kikosi cha Brazil tangu kocha wa sasa wa nchi hiyo Tite achukue mikoba ya kuinoa miamba hiyo msimu uliopita.
Luiz ameliambia gazeti la Evening Standard kuwa ameumia kutokuwemo kikosini kwa mara nyingine lakini anaheshimu maamuzi ya kocha.
Akijibu swali baada ya kuulizwa kama alishawahi kuambiwa sababu ya kutojumuishwa kwake kikosini,Luiz amesema hapana na kuongeza kuwa bado anaamini kuwa iko siku atarejea tena kikosini.
0 comments:
Post a Comment