Monaco,Ufaransa.
Kinda nyota wa klabu ya Monaco, Kylian Mbappe na straika wa Lyon, Alexandre Lacazette ni wachezaji wawili ambao wapo juu ya orodha ya usajili wa klabu ya Arsenal majira ya kiangazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Mirror.
Gunners wanakabiliwa na kazi kubwa ya kujenga kikosi chao kama Mesut Ozil na Alexis Sanchez wataondoka - na wote wawili hao bado hawajasaini mikataba mipya hasa baada ya kutofahamu mustakabali wa kocha Wenger.
Kama Ozil na Sanchez wakiondoka, Arsenal watavunja benki majira ya kiangazi ,huku Borussia Dortmund Marco Reus na mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele wakiwa kwenye rada yao.
0 comments:
Post a Comment