728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 26, 2017

    Msuva amwagia sifa lukuki Mbwana Samatta



    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WINGA mahiri wa Taifa Stars,Simon Msuva amemwagia sifa lukuki nahodha wa timu hiyo ,Mbwana Samatta kwa kusema kuwa mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji ni mfano bora kwa wachezaji wazawa.

    Jana Jumamosi Samatta aliifungia Taifa Stars mabao mawili na kuiwezesha kuifunga Botswana mabao 2-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Akiongea na mtandao huu,Msuva amesema Samatta ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu mkubwa wa michezo ya kimataifa na uwepo wake uwanjani umekuwa ukiwapa nguvu ya kupambana kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.

    Anajua afanye nini katika wakati upi.Ni mchezaji wa kipekee sana,tunaona fahari kuwa nae kikosini.

    Wakati huohuo Msuva ambaye ni kinara wa upachikaji mabao ligi kuu bara,ameongeza kuwa wachezaji wazawa wanapaswa kucheza kwa bidii na kumtumia Samatta kama chachu ya kufikia malengo yao.

    Amesema kuwa na kipaji pekee haitoshi na badala yake wanapaswa kujipambanua kwa kucheza kwa bidii kubwa na maarifa.Ameongeza ili Tanzania iweze kupambana na mataifa kama Senegal,Cameroon na Misri inapaswa kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje ya nchi.

    Taifa Stars itarejea tena dimbani kesho kutwa Jumanne kucheza na Burundi kwenye mchezo wake wa pili wa kimataifa wa kirafiki.Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Msuva amwagia sifa lukuki Mbwana Samatta Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top